Header Ads

Uvamizi, ukataji wa Miti ovyo hatarini kuupoteza Msitu wa Ngezi


Image result for msitu wa ngezi VITENDO vya uvamizi na ukataji wa Miti ndani ya hifadhi ya msitu wa  Serikali  Ngezi unaofanywa na baadhi ya wanajamii, ni miongoni wa uharibifu wa mazingira na unaweza kusababisha kupotea  asili ya msitu huo.
Hayo yamesemwa na Afisa Mkuu wa Idara ya Misitu, na Maliasili zisizorejesheka kisiwani Pemba, Said Juma Ali,baada ya kutokea uvamizi wa kukatwa mti mkubwa, aina ya Mivule,  ndani ya hifadhi ya msitu wa Ngezi.
Amesema kuwa msitu kwa kipindi umekuwa ukichangia uchumi wa nchi, kupitia watalii wanaokuja kutalii ndani ya hifadhi hiyo.
 Aidha Mkuu huyo wa IDARA amesema, mmoja wa wahalifu  ni mzoefu wa vitendo vya kuuhujumu msitu huo, na kuviomba vyombo vya sheria kumkamata mtuhumiwa huyo, kabla hajakimbia.
Kwa upande wake Mkuu wa hifadhi ya msitu wa Ngezi ,Abdi Mzee Kitwana amesema ,licha ya wahalifu kufanikiwa kukimbia, lakini aliweza kuwatambua majina yao na sehemu wanazoishi.

No comments