Header Ads

SMZ yawaonya Walimu wakuu Matumizi ya Fedha za Serikali

WALIMU wakuu wa skuli za serikali wametakiwa kuzitumia fedha zilizotengwa kwenye mradi wa kuimarisha elimu ya wanafunzi wa serikali (ZISP) ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zazibar, Madina Mjaka Mwinyi, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu wakuu wa skuli za serikali na binafsi katika ukumbi wa skuli ya Haile Selassie mjini Unguja.

Alisema, lengo la fedha hizo ni kutumika kwa kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa utulivu sambamba na kupata matokeo mazuri ya mitihani ya kitaifa.

Aidha aliwahimiza walimu kuwa na mpango kazi wa matumizi sahihi ya fedha watakazokabidhiwa kwa ajili ya kununulia vifaa wanavyovihitaji na kuainisha vizuri mahitaji yao.

Aliwataka kushirikiana pamoja na kamati za skuli kupanga mpango kazi na mikakati ya kuimarisha elimu katika skuli ili lengo la kupata matokeo mazuri liweze kufikiwa.

No comments