Waziri SMZ: 'huduma usafishaji Figo ‘Dialysis’ katika Hospitali ya Mnazimmoja zitaendelea kutolewa bila ya malipo'
WAZIRI wa Afya, Hamad Rashid Mohammed amesema huduma usafishaji
figo ‘dialysis’ katika hospitali ya Mnazimmoja zitaendelea kutolewa bila ya
malipo.
Waziri huyo alieleza hayo katika hospitali ya Mnazimmoja wakati
alipofanya ziara kukitembelea kitengo cha huduma za usafishaji figo na kueleza
kuwa huduma hizo zitaendelea kutolewa bure.
Alisema lengo la ziara yake katika kitengo hicho, ni kuona jinsi
wananchi wanavyofaidi na huduma hizo, hasa ikizingatiwa kuwa serikali inataka
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za afya za uhakika ndani ya nchi.
Aidha alisema serikali kupitia wizara ya Afya kwa kuwajali
wananchi iko imara katika kuhakikisha inakipa kipaumbele kwa kukipatia vifaa
kitengo hicho pamoja na dawa kwa wagonjwa wanaofika kwenye kitengo hicho
kusafishwa figo.
Post a Comment