Rais Xi Jinping aongoza mkutano wa kilele wa Jumuiya ya SCO
MKUTANO
wa 18 wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai umefunguliwa leo asubuhi
huko Qingdao, mashariki mwa China.
Rais
Xi Jinping wa China, ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo, ameongoza mkutano
wa wakuu wa nchi nane wanachama, ambazo ni China, Russia, Kazakhstan,
Kyrgyzstan, Tajikistan, Uzbekistan, India na Pakistan.
Huu
ni mkutano wa kwanza wa kilele tangu jumuiya hiyo ikubali uanachama wa India na
Pakistan mwaka jana.
Habari
zinasema, viongozi hao watabadilishana maoni kuhusu hali ya jumuiya hiyo,
ushirikiano kati ya nchi wanachama na masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.
Pia
watasaini Azimio la Qingdao pamoja na nyaraka zaidi ya 10 zinazohusu
ushirikiano katika nyanja za usalama, uchumi na utamaduni.
Post a Comment