Idara ya Maendeleo ya Mifugo Pemba yavuka lengo la WHO Chanjo ya Mbwa
LICHA
ya ushiriki mdogo wa wafugaji wa mbwa kupeleka mbwa wao kupatiwa chanjo
ya kichaa cha mbwa , lakini Idara ya Maendeleo ya Mifugo kisiwani Pemba
imefanikwa kuvuka lengo la kutoa chanjo lililowekwa na Shirika la Afya
Ulimwenguni –WHO- kwa mwaka 2017.
Akizungumza
wakati wa zoezi la kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa katika kisiwa cha
fundo , Daktari wa mifugo Ali Zahran Mohammed kwa niaba ya Mkuu wa Idara
ya Maendeleo ya Mifugo Pemba , amesema Idara imefanikiwa kupunguza kesi
za watu kutafunwa na mbwa kutoka 289 kwa mwaka 2017 mpaka kesi 26
kwa mwaka huu.
Aidha
Dr Ali amesema bado zipo changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja
na wananchi kutowapeleka mbwa wao kupatiwa chanjo hususani wafugaji wa mbwa wa
wilaya ya michezweni .
Naye
mfugaji wa mbwa yussuf abeid sharif amewataka wafugaji wenzake wa mbwa
kushiriki kuwapeleka mbwa wao kuwapatia chanjo hiyo ili kuwakinga na ugonjwa wa
kichaa cha mbwa .
Zaidi
ya mbwa 2000 wanatarajia kupatiwa chanjo ya kinga ya kichaa cha mbwa kwa wilaya
zote za Pemba.
Post a Comment