OTHMAN MASOUD: ATHARI ZA KIMAZINGIRA ZINAZOTOKANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI BADO NI TISHIO KUBWA LA KIMAZINGIRA ZANZIBAR
Zanzibar,
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba athari za kimazingira
zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi bado ni changamoto na tishio kubwa la kimazingira linaloendelea
hapa Zanzibar licha ya serikali kufanya juhudi kadhaa kukikabili hali hiyo.
Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake
Migombani mjini Zanzibar alipokutana na
Ujumbe wa Shirika Aga Khan Foundation ulioongozwa na Mtendaji Mkuu wa Kanda ya
Afrika Mashariki wa Shirika hilo hilo Riaz Nathu.
Kikao hicho kililenga kufanya mashauriano ya
mashirikiano juu ya masuala mbali mbali yaliyochini ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza
wa Rais ikiwemo suala la changamoto ya mazingira, madawa ya kulevya, Ukimwi na
mabadiliko ya Tabia nchi ambayo ni masuala mtambuka yanayosimamiwa na ofisi
hiyo.
Mhe. Othman amesema kwamba athari
zinazotokana na janga la kimazingira linaendelea kuwa changamoto kubwa duniani
hasa katika nchi za Visiwa ikiwemo Zanzibar ambapo maeneo mbali mbali zikiwemo
fukwe hasa katika kanda za utalii Unguja na Pemba yanaendelea kuharibika
kutokana na athari za kimazingira.
Amefahamisha kwambva hivi sasa
katika maeneo kama vile ya Jambiani , Nunguwi na sehemu nyengine za Pemba kama
vile Tovuni Kaskazini Pemba ni miongoni mwa maeneo ambayo mmongonyoko wa fukwe unaendelea kuathiri maeneo hayo licha ya
jitihada mbali mbali za serikali na washirika wa maendeleo zinazochukuliwa
kukabiliana na hali hiyo kuendelea.
Mhe. Makamu amesema kwamba hata hivyo , jitihada za Serikali zimesaidia
wakulima zaidi ya 200 wa Bonde la Tovuni Kiungoini Pemba kurejea katika mashamba yao kuaendelea
na shughuli zao za kilimo cha mpungu wa kutegemea mvua
ambapo kabla ya juhudi hizo wakulima hao walishindwa kuendeleza kazi ya
kilimo hicho kutokana na mashamba hayo
kuingiwa na maji ya chumvi.
Amefahamisha kwamba hatua ya
kuwarejesha wakulima hao kuendelea na kilomo cha mpunga katika bonde hilo la
tovuni ni mafanikio makubwa ambapo pia ni matokeo ya
juhudi za serikali na washirika mbali mbali wa maendeleo katika kusaidiana kuzikabili ipasavyo
changamoto na athari za mabnadiliko ya tabia nchini.
Amesema kwamba kutokana na hali
hiyo serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuwakaribiasha na ipo tayari
kushirikiana na washirika mbali mbali wa maendeleo katika kuasaidia juhudi za pamoja za kukabilia
hali hiyo na kuweza kupunguza athari zinazoendelea.
Amefahamisha kwamba hivi Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kutekeleza Mradi mkubwa wa Kitaifa wa
kuirejesha Zanzibar kuwa ya Kijani ambapo juhudi za serikali na washirika wa maendeleo
zinahitajika sana kuunga nguvu katika kufanikisha utekelezaji wa suala hilo.
Ameufahamisha ujumbe huo kwamba
dhamira ya Serikali katika mradi huo ni
kuwajenga wanajamii wa Zanzibar kuanzia watoti maskulini kupanda na kuithamini
miti ya aina mbali mbali kuiwezesha
Zanzibar kuwa ya kijani ambapo shughuli hiyo inakusudia kuwa shirikishi kwa
wadau mbali mbali wakiwemo wananchi na mashirika ya aina tofauti kama vile shirika la Aga Khan Foundation.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
Aga Khan Kanda ya Afrika Mashariki Riaz Nathu, ameipongeza serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zake inazozishukua katika kukabiliana na
suala hilo pamoja na kuwakaribisha washirika wa maendeleo kusaidiana na juhudi
hizo katika kukabiliana na changamoto
zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchini.
Amefahamisha kwamba kutona na hatua
hiyo Shirika la Aga Khan Foundation nalo lipo tayari kuendelea kushirikiana na
Zanzibar katika maeneo mbali mbali ili kwa pamoja kupunguza athari zitokanazo na
chamgamoto ya Mabadiliko ya tabia nchi.
Post a Comment